KITENGO CHA ANWANI ZA MAKAAZI NA MISIMBO YA POSTA

Serikali ya Tanzania kupitia Sera ya Taifa ya Posta iliyoidhinishwa mwaka 2003, imedhamiria kuanzisha mfumo wa anwani zinazoendana na majina ya mitaa ambapo watu binafsi na maeneo ya biashara yatatambulishwa kwa kutumia majina ya maeneo yaliyopo pamoja na msimbo wao wa posta.

Anwani hizi za makaazi zilizinduliwa rasmi na aliyekuwa Makamo wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Ali Mohamed Shein mnamo tarehe 18/01/2008 Clock-Tower Area Arusha Tanzania.Kwa ujumla, anwani ni njia ya msingi ya kubainisha na kutambua mtu/kitu mahususi kilipo.

Mfumo wa uundaji wa anwani za makazi ni zoezi linalowezesha kutambua eneo kwa kulipatia namba ya msimboposta, majina ya barabara na namba za nyumba, kupitia mpango maalumu unaobainishwa katika viwango vya taifa na kutunza taarifa hizi katika hifadhi-data. Mfumo huu hautakuwa na marudiorudio, kuachwa kwa taarifa muhimu, maelezo marefu sana na ukosefu wa uthabiti katika utambuzi wa maeneo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mfumo wa anwani wa Sanduku la Posta una dosari kadhaa ukilinganishwa na mfumo wa anwani za makazi na hasa katika ubainishaji sahihi wa watu na uwezeshaji wa biashara na utoaji wa huduma za kijamii. Anwani ya makazi, inaruhusu watu kufika, kubainisha na kufikia maeneo fulani muhimu katika mji au makazi. Mtu anahitaji anwani ya makazi ili kutambuliwa kama mtu binafsi, raia au mteja.

Mfumo mpya wa uundaji wa anwani utahakikisha kwamba:-

Kila mtu anayeishi Tanzania ana anwani halisi ya makazi Kila biashara inayosajiliwa Tanzania ina anwani halisi ya makazi Usajili wa mali, biashara, vizazi na vifo unaboreshwa Huduma za dharura, kama vile polisi, zimamoto na magari ya wagonjwa, zinaweza kutambua maeneo yenye dharura na kuyafikia kwa haraka Wageni wanaweza kubaini mahali wanakokwenda kirahisi Mamlaka za Mapato zinabaini walipa kodi kirahisi Makampuni yanayotoa huduma kwa umma yanaboresha huduma zao Muda mfupi unatumika katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi ikiwa ni pamoja na huduma za posta na za safari.

UTEKELEZAJI KWA UPANDE WA ZANZIBAR

Zoezi la majaribio kwa upande wa Zanzibar limefanyika Wilaya ya Magharibi katika Shehia za Chukwani na Mombasa kwa Unguja. Kwa upande wa Pemba zoezi kama hili limefanyika katika Shehia za Limbani na Selem, pia kulazimika kuendelea katika shehia za Kipangani, Bopwe, Kizimbani, Utaani na Jadida katika Wilaya ya Wete kutokana na sababu za kijografia. Aidha zoezi hili lilifanyika katika shehia za Mkanyageni, Chokocho na Michenzani katika Wilaya Ya Mkoani Pemba kwa hatua ya uwekaji wa majina ya mitaa tu.

NYUMBA ZILIZOWEKEWA NAMBA

Uwekaji wa vibao vya namba za nyumba kwa Zanzibar umefanyika katika shehia tisa ambazo ni Mombasa na Chukwani kwa Unguja na Limbani, Selem, Kipangani, Bopwe, Mtemani, Utaani na Jadida kwa Pemba. Jumla ya vibao 5985 vya nambari za nyumba vimewekwa Unguja na Pemba, ambapo vibao 4368 vimewekwa Unguja na 1617 Pemba

NGUZO ZA MAJINA YA MITAA

Uwekaji wa nguzo za majina ya mitaa umefanyika katika shehia 14 Unguja na Pemba, ambazo ni Chukwani, Mombasa, Tomondo na Kiembesamaki kwa upande wa Unguja na kwa upande wa Pemba ni shehia za Limbani, Selem, Kipangani, Bopwe, Kizimbani, Utaani na Jadida katika Wilaya ya Wete Pemba na Mkanyageni, Chokocho na Michenzani katika Wilaya ya Mkoani Pemba. Jumla ya nguzo za majina ya mitaa 197 zimewekwa Unguja na Pemba ambapo Unguja nguzo 105 na kwa upande wa Pemba nguzo 92 .

UWASILISHWAJI TARIFA YA POSTCODE SERIKALINI

Taarifa ya mradi wa postikodi iliwasilishwa katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar siku ya Jumanne 14/04/2015 ambapo ilipokelewa na kupitishwa. Aidha tarifa hiyo imeshapitishwa na Baraza la Mapinduzi tarehe 16/07/2015.

UINGIZWAJI WA TAARIFA KATIKA HIFADHIDATA YA KITAIFA (NAPS)

Taarifa za anwani za makaazi zinaendelea kuingizwa katika hifadhi data ya kitaifa kama zinavyo onekana katika mtandao www.address.go.tz.

UINGIZWAJI WA TAARIFA KATIKA HIFADHIDATA YA KITAIFA (NAPS)

Taarifa za anwani za makaazi zinaendelea kuingizwa katika hifadhi data ya kitaifa kama zinavyo onekana katika mtandao www.address.go.tz. Maeneo yenye rangi za manjano, nyekundu au bluu ni maeneo ambayo tayari tarifa za wakaazi wake zimeshaingizwa kwenye hifadhi data ya Taifa, ambapo maeneo yenye rangi nyeusi na mistari hayajaingizwa. Kwa kupata Anuwani ya Postikodi ya eneo unaloishi bonyeza hapa https://www.address.go.tz/postcode/Home/Home.do

Kwa kupata orodha kamili ya Postikodi bonyeza hapa http://www.tcra.go.tz/index.php/publication-and-statistics/postcode-list

Kurasa za Karibu

  • Habari na Matukio
  • Dira na Dhamira
  • Majukumu ya Idara
  • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.