UFUNGAJI WA VIDEO CONFERENCE ZANZIBAR:

Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ya Tanzania kwa kuzingatia umuhimu wa kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa wananchi, imeamua kufunga video conference kwenye mikoa yote ya Tanzania zikiwemo Ikulu. Kwa upande wa Zanzibar mradi huu umewekwa kwenye ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za mikoa husika. Vituo vilivyofungwa video conference hizo kwa kuzingatia mahitaji ni:

  1. Ikulu kwa ajili ya mawasiliano ya Rais
  2. Wizara ya Miundimbinu na Mawasiliano (Kisauni, Mjini Magharibi)
  3. Chuo cha Mafunzo ya Amali (Mkokotoni, Kaskazini Unguja)
  4. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Chakechake, Kusini Pemba)
  5. Wizara ya Uvuvi na Mifugo (Wete, Kaskazini Pemba)

Vituo hivyo vilivyowekwa ni kwa ajili ya mawasiliano ya Taasisi zote za Serikali pamoja na Taasisi binafsi pale watakapohitaji kutumia.Aidha Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ndie msimamizi wa Video Conference hizo kwa upande wa Zanzibar, na tayari vituo hivyo vinafanya kazi kwa kutumia Internet. Kwa kuwa mkonga wa mawasiliano tayari umeshafika katika vituo hivyo vya video conference Wizara inafuatilia kuweza kutumilia mtandao wa ndani yaani Intranet kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa mawasiliano, na mara tu baada ya kukamilika zoezi hilo vituo hivyo vitazinduliwa rasmi na kuanza kutumika.

UJENZI WA VITUO MAHIRI VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBU (DATA CENTRE):

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inaendelea na utekelezaji wa mradi wa mkonga wa Taifa Awamu ya tatu baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza na ya pili. Awamu yay a tatu itahusisha ujenzi wa vituo mahiri vya kutunzia kumbukumbu (Internet Data Centre) katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Aidha itajengwa pia Miundombinu ya itifaki ya kuunganisha huduma mbalimbali za mawasiliano [Internet Protocol-Multiprotocol Label Switching (IP-MPLS) Network] ili kufanya mkonga wa Taifa wa mawasiliano uweze kutoa huduma vyema na bora zaidi.

Ili kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho cha kutunzia kumbukumbu Zanzibar, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iilikabidhiwa jukumu la kutafuta kiwanja cha kujenga kituo hicho na kuletwa wataalam kufanya tathmini ya mazingira (Environmental Impact Assessement) katika eneo litakalojengwa kituo hicho.

Katika kufanikisha kazi hii Idara ya Mawasiliano iliwasilisha maombi kwa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa ajili ya kutupatia kiwanja hicho. Na ZIPA walikubali kutupatia kiwanja eneo la Fumba kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Idara pia iliwasiliana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, kwa ajili ya kuomba kufanya tathmini ya mazingira (Environmental Impact Assessement) katika eneo litakalojengwa kituo hicho. Ambapo walitupatia muongozo na kufanikisha zoezi hilo ikiwa ni pamoja upatikanaji wa cheti cha mazingira. Wataalam walitumwa kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na kufanya tathmini hiyo.

Kituo kimoja kimeshaanza kujengwa na kinaendelea cha Dar es Salaam na vituo vyengine Dodoma na Zanzibar vipo kwenye mchakato kwa ajili ya ujenzi huo.

Kurasa za Karibu

  • Habari na Matukio
  • Dira na Dhamira
  • Majukumu ya Idara
  • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.