MKONGA WA MAWASILIANO WA TAIFA Idara ya Mawasiliano iliyopo chini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ndiyo iliyokabidhiwa jukumu la kusimamia mkonga wa mawasiliano wa Taifa na kuhakikisha Serikali inafaidika kutokana mradi huo. Kutokana na mkataba wa makubaliano ya mashirikiano yaliyosainiwa tarehe 15 mwezi wa Febuari 2013 baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Zantel kwa ajili ya uwekaji na uunganishaji wa mkonga wa mawasiliano. Kiambatanisho namba moja kiliitaka Zantel kuzifikishia na kuziunganisha mkonga Taasisi 84 za Serikali.

Uunganishaji wa mkonga kwa Taasisi za Serikali:

Jumla ya Taasisi 84 Unguja na Pemba zimefikishiwa mkonga wa mawasiliano kwa hatua ya Optical Distribution Frame (ODF) kati ya hizo hamsini na nne (54) zimeshafungiwa vifaa vya mkonga wa mawasiliano kwa hatua ya matumizi kwa upande wa Unguja na tayari zinaonana na makao makuu ya Serikali mtandao Mazizini Zanzibar ikijumuisha na Wizara ya Ardhi Pemba. Aidha Idara ya Mawasiliano ipo mbioni kuhakikisha zoezi linaendelea kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel pamoja na Idara ya Serikali Mtandao (E-Government) ya kuhakikisha Taasisi zilizobaki kwa upande wa Pemba zinapatiwa vifaa vya kuziunganisha na kuziwezesha kupata huduma zilizokusudiwa.

Kurasa za Karibu

  • Habari na Matukio
  • Dira na Dhamira
  • Majukumu ya Idara
  • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.