KITENGO CHA MINARA
Kitengo hichi kina jukumu la kusimamia ujenzi na utunzaji wa minara ya mawasiliano hapa Zanzibar. Kitengo hichi kinajumuisha wajumbe kutoka taasisi mbali mbali zikiwemo.
- Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji.
- Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
- Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati,
- Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
- Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
- Mamlaka ya Viwanja vya ndege
- Wizara ya habari
Miongoni mwa kazi zinazofanywa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa maeneo mapya yanayotaka kujengwa minara, na kutoa ruhusa ya ujengaji huo.