Idara ya Mawasiliano

Idara ya Mawasiliano ni idara inayoandaa , kuboresha na kusimamia sera ya TEHAMA na kutoa ushauri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yote yanayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano Zanzibar.Idara hii ina jukumu la kusimamia huduma za mawasiliano na masuala ya Taasisi za Mawasiliano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zilizopo Zanzibar. Idara pia, ina jukumu la kuratibu na kusimamia uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano. Idara inaendelea kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa Zanzibar, kuendelea kuandaa Sheria na Kanuni za TEHAMA na Mpango Mkakati wa TEHAMA. Idara pia ina jukumu la kusimamia mkonga wa mawasiliano kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel kwa upande wa matumizi ya Serikali na Taasisi binafsi.

TAASISI ZA MUUNGANO SEKTA YA MAWASILIANO

Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imeendelea kushirikiana na Taasisi za Muungano zilizopo hapa Zanzibar katika utoaji wa huduma na usimamizi wa Sekta ya Usafiri na Mawasiliano. Miongoni mwa Taasisi za Muungano tunazoshirikiana nazo ni:- Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania (TMA), Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA), Shirika la Posta la Tanzania (TPC) na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA). Mashirikiano naTaasisi yamechangia sana kukuza Sekta ya Usafiri na Mawasiliano hapa Zanzibar.

MAFANIKIO YA IDARA YA MAWASILIANO..

Idara ya Mawasiliano inasimamia na kuimarisha huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano hapa Zanzibar.Idara imefanya matengenezo ya mkonga wa taifa maeneo yalioharibika katika barabara ya Tunguu – Istiqama, Kiwengwa, Paje na Nungwi Unguja. Kwa upande wa Pemba hatua za matengenezo zinaendelea katika maeneo mbali mbali kama vile Machomane, Wete, Kwale, Kizimbani, Kiungoni na Kifumbikai zimekamilika.Aidha, uwekaji “Alarm System” kwenye vituo vyote 12 vya mkonga vilivyopo Zanzibar umefanyika ili kuvilinda na kuviwezesha kutoa taarifa Makao Makuu pale maharibiko ya aina yoyote yatakapotokezea.

kuhusu uunganishwaji wa Mkonga kwenye taasisi za Serikali, hadi kufikia Machi 2015, taasisi 84 tayari zimeunganishwa na mkonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Zantel, ikiwa taasisi 50 zinatumia huduma hiyo na taasisi 34 zipo katika hatua za mwisho za kuwekewa vifaa husika ili nazo ziweze kutumia huduma hii.

Wizarakwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ya SMT imeweka mitambo ya mawasiliano picha (Video Conference) katika sehemu 5 tofauti Unguja na Pemba na mitambo hiyo inafanya kazi. Aidha, Wizara kwa kushirikia na Kampuni ya ZTE ya China imefunga computer 50 kwa ajili ya Kituo Jamii cha TEHAMA katika skuli ya Kiembe Samaki na kuunganishwa na mkonga wa Taifa.

 

Kurasa za Karibu

  • Habari na Matukio
  • Dira na Dhamira
  • Majukumu ya Idara
  • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.