Muendelezo wa Mafunzo kwa Masheha juu ya uelewa na utunzaji wa mkonga wa mawasiliano
27 Nov 2018

Muendelezo wa Mafunzo kwa Masheha juu ya uelewa na utunzaji wa mkonga wa mawasiliano

namba moja

Afisa wa Idara ya Mawasiliano Eng Abass Juma Yahya akiwasilisha kwa masheha umuhimu wa miundombinu ya Mkonga wa mawasiliano uliopitishwa katika Shehia Mbali Mbali.

maswali

Sheha wa shehia ya Kibondeni Ndugu Iddi A. Hajji  akiuliza maswali juaa ya mada zilizotolea katika mafunzo hayo.

namba mbili

Sheha wa shehia ya Fuoni Migombani Ndugu Ramadhan M. Khatib  akiuliza maswali juaa ya mada zilizotolea katika mafunzo hayo.

 

Muendelezo wa Mafunzo ya Uelewa na Utunzaji wa Miundombinu ya Mkonga wa Mawasiliano kwa Masheha tarehe 27/11/2018 katika ukumbi wa Wizara Kisauni.

Katika kuhakikisha mkonga wa mawasiliano unahifadhiwa na kutunzwa kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yaliyolazwa mkonga Zanzibar, Idara ya Mawasiliano imetoa mafunzo ya siku mbili tarehe 27 hadi 28/11/2018 kwa masheha pamoja na kuwakaguza njia zilizopitishwa mkonga na kuwaelimisha kwa kina uwepo wa miundombinu ya mkonga wa mawasiliano katika shehia zao na umuhimu wa kuihifadhi miundombinu hiyo kwa mustakbali nzuri wa maendeleo endelevu ya nchi yetu kiuchumi na kijamii.

Aidha wametakiwa Masheha hao wahakikishe kwamba wanawafikishia mafunzo hayo wananchi katika shehia zao juu ya uwepo wa miundombinu hiyo na kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo, pamoja nakutoa taarifa kwa Idara husika pale watakapoona hujuma inafanyika katika shehia zao.

Masheha waliopatiwa mafunzo kwa njia (route) ya mkonga kutoka ID Card Mazizini hadi shehia ya Kibondeni ni hawa wafuatao: -

 1. Sheha wa Shehia ya Mombasa
 2. Sheha wa Shehia ya Kwa Mchina
 3. Sheha wa Shehia ya Sokoni
 4. Sheha wa Shehia ya Meli nne
 5. Sheha wa Shehia ya Kwerekwe
 6. Sheha wa Shehia ya Taveta
 7. Sheha wa Shehia ya Pangawe
 8. Sheha wa Shehia ya Kijito Upele
 9. Sheha wa Shehia ya Uwandani
 10. Sheha wa Shehia ya Migombani
 11. Sheha wa Shehia ya Chunga
 12. Sheha wa Shehia ya Kibondeni

 

Last modified on Wednesday, 28 November 2018 09:38

Kurasa za Karibu

 • Habari na Matukio
 • Dira na Dhamira
 • Majukumu ya Idara
 • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.