Mafunzo kwa Masheha juu ya uelewa na utunzaji wa mkonga wa mawasiliano yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara Kisauni.
05 Oct 2018

Mafunzo kwa Masheha juu ya uelewa na utunzaji wa mkonga wa mawasiliano yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara Kisauni.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Dkt. Mzee Suleiman Mndewa akiwasilisha kwa masheha umuhimu wa miundombinu ya Mkonga wa mawasiliano uliopitishwa katika Shehia Mbali Mbali.

Masheha wakipokea kwa makini  ufafanuzi wa umuhimu wa  Miundombinu ya mawasiliano ya Mkonga .

Mafunzo ya Uelewa na Utunzaji wa Miundombinu ya Mkonga wa Mawasiliano kwa Masheha tarehe 04/10/2018 katika ukumbi wa Wizara Kisauni.

Katika kuhakikisha mkonga wa mawasiliano unahifadhiwa na kutunzwa kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yaliyolazwa mkonga Zanzibar, Idara ya Mawasiliano imetoa mafunzo ya siku mbili tarehe 04 hadi 05/10/2018 kwa masheha pamoja na kuwakaguza njia zilizopitishwa mkonga na kuwaelimisha kwa kina uwepo wa miundombinu ya mkonga wa mawasiliano katika shehia zao na umuhimu wa kuihifadhi miundombinu hiyo kwa mustakbali nzuri wa maendeleo endelevu ya nchi yetu kiuchumi na kijamii.

Aidha wametakiwa Masheha hao wahakikishe kwamba wanawafikishia mafunzo hayo wananchi katika shehia zao juu ya uwepo wa miundombinu hiyo na kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo, pamoja nakutoa taarifa kwa Idara husika pale watakapoona hujuma inafanyika katika shehia zao.

Masheha waliopatiwa mafunzo kwa njia (route) ya mkonga kutoka ID Card Mazizini hadi Fumba ni hawa wafuatao:-

 1. Ndugu Hassan Moh’d Mataka – Shehia ya Mbweni
 2. Ndugu Zahor Moh’d Zahor – Shehia ya Kiembe Samaki
 3. Ndugu Fauzia Omar Mahawi – Shehia ya Michungwani
 4. Ndugu Hija Suleiman Othman – Shehia ya Kisauni
 5. Ndugu Ali Kibwana Juma – Shehia ya Maungani
 6. Ndugu Mussa Khamis Mussa – Shehia ya Kombeni
 7. Ndugu Khatibu Ame Baraka – Shehia ya Dimani
 8. Ndugu Haruna Migoda Mataka – Shehia ya Bweleo
 9. Ndugu Issa Hassan Shoka – Shehia ya Fumba
Last modified on Friday, 05 October 2018 09:13

Kurasa za Karibu

 • Habari na Matukio
 • Dira na Dhamira
 • Majukumu ya Idara
 • Vitengo vya Idara

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.